Mwili wa Dk. Raymond Simion ukitolewa kwenye chumba cha kulala wageni na polisi.
Taarifa kutoka katika gesti hiyo zinasema marehemu alijiorodhesha
kwenye kitabu cha wageni kuwa ni daktari wa Hosptali ya Nyamagana jijini
Mwanza na alikuja Dar kikazi kwa muda wa wiki moja. Mauti yalimkuta
akiwa na siku mbili tu tangu alipowasili.Mmoja wa wahudumu wa gesti hiyo ambaye hakupenda jina lake litajwe gazetini alisema kuwa, daktari huyo alifika katika gesti hiyo Jumapili ya Mei 4, mwaka huu na kuchukua chumba namba 102.
Alisema Jumatatu ya Mei 5, marehemu aliomba abadilishiwe chumba, akapewa namba 105 ambamo mauti yalimkutia.
Mwili wa Dk. Raymond Simion ukipakizwa kwenye gari la polisi.
Uwazi lilifanikiwa kufika katika eneo la tukio na kufanya mahojiano
na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Ubungo NHC, Amani Sizian ambaye
alisema taarifa ya kifo cha daktari huyo aliipokea saa 9: 03 alasiri ya
siku ya tukio ambapo mhudumu wa gesti hiyo ndiye aliyempigia simu
kumjulisha.Kiongozi huyo aliendelea kusema kuwa mhudumu huyo alimweleza kwamba marehemu baada ya kuchukua chumba Jumapili alitoka na kurudi saa 3:00 usiku ambapo alilala, lakini kesho yake hakuonekana kutoka.
Nje ya eneo la tukio.
“Mhudumu aliniambia kuwa baada ya kutomwona asubuhi, hawakumfuatilia
hadi ilipofika saa 9:00 alasiri ambapo walikwenda kumchungulia chumbani
kwake na kumwona katika hali ya kutokuwa hai.“Ilibidi niende. Nilipofika tukakuta mlango umefungwa kwa ndani.
Katika kumchungulia tulimwona mtu huyo akiwa amekaa kitandani bila kujigeuza jambo lililonifanya nipige simu polisi ambao walifika na kuvunja mlango na kumkuta akiwa amefariki dunia,” alisema mwenyekiti huyo.
Aliongeza kuwa, katika chumba hicho alichofia mteja huyo, kulikutwa mabomba mawili ya sindano ambapo moja lilikwishatumika, pia kulikuwa na mifuko miwili yenye nguo na begi moja.
Polisi waliuchukua mwili na kuupeleka Hospitali ya Taifa Muhimbili. Hata hivyo, ndugu wa marehemu walipatikana na mwili kufanyiwa uchunguzi na daktari kisha kuuchukua na kuusafirisha kwenda Mwanza kwa mazishi.
Chumba alipokuwa amelala marehemu Raymond Simion.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP Camilius Wambura
alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema: “Marehemu alikutwa na
mabomba mawili ya sindano, moja lilishatumika na lilikuwa na masalia ya
damu. Pia kulikuwa na kete moja ya vitu vinavyodhaniwa kuwa ni madawa ya
kulevya.