Mchungaji Christopher Mtikila amechafua hali ya hewa bungeni, kwa kumtaka Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Pandu Kificho amueleze ni kwanini tangu jana amekuwa akimnyima nafasi ya kuzungumza bungeni.
Mchungaji Mtikila alisimama ghafla na kusema: Mwenyekiti kwanini
unaninyima haki yangu ya kuzungumza, nataka kujua kwanini unaninyima
haki ya kuzungumza. Kuzungumza ni haki yangu."
Mchungaji Mtikila amezungumza kwa jazba huku wajumbe wengine
wakimzomea, lakini bila uwoga aliendelea kuzungumza na kusema
yanayofanyika Mungu anapenda na yeye ana amini katika Mungu, lakini
"Wewe Mwenyekiti inaonekana kuwa hupendi Mungu."
Wakati Mchungaji Mtikila akimwakia Kificho, Felix Mkosamali alilipuka
na kumwambia mwenyekiti kuwa tangu jana pia anamnyima nafasi.
"Ninyi mmejipanga, kupitisha kanuni mbovu, alafu sisi wengine hamtupi nafasi," amesema Mkosamali.
Mwenyekiti Kificho aliwajibu kuwa kwa bahati mbaya wamekosa nafasi na hivyo wawe wavumilivu.
Kificho anatangaza utaratibu wa kumchagua Mwenyekiti wa kudumu wa
Bunge na wajumbe wanaotaka kugombea nafasi hiyo wametakiwa kuchukua fomu
ya kugombea.
Bunge hilo limeahirishwa mpaka kesho na kanuni zitaanza kufanya kazi rasmi.
