BAADA YA KUPATA MTOTO, MTITU AWASHUKURU MADAKTARI

 
Mke wa Mtitu, Jovitha Swai akiwa na mwanaye.
MSANII wa filamu ambaye pia ni prodyuza, William Mtitu, amewashukuru madaktari kwa kumsaidia mkewe, Jovitha Swai kujifungua salama mtoto wao. Jovitha Swai alijifungua jana mtoto wa kike.

Kupitia katika ukurasa wake wa Facebook, Mtitu ameandika hivi: "Nawashukuru madaktari wa Hospitali ya Regency na kwa Dk. Mvungi wakiongozwa na Dk. Getu kwa kusaidia mpaka mke wangu kujifungua salama na sasa naitwa baba na mke wangu mama. Kwa kweli Mungu awabariki sana."
Mtitu na mkewe Jovitha walifunga ndoa Septemba 8, mwaka jana katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, jijini Dar es Salaam na baadaye sherehe ikafanyika  ukumbi wa Urafiki, Ubungo. GPL inamtakia mtoto wa Mtitu maisha mema!
back to top