Wema Sepetu miss Tanzania aliyegeuka kuwa
muigizaji, ameweka wazi kwamba anataka kuimba na katika kuthibitisha
hilo ameshaandika mistari kadhaa ya anachotaka kuimba. Wema alishawahi
kuimba kwenye wimbo wa kuhamasisha kumchangia msanii Sajuki wakati
anaumwa. Wimbo huo unaitwa “Mboni yangu”, so kuingia kwenye booth
kurekodi wimbo sio kitu kipya kwa Wema Sepetu.
Hii ni baadhi ya mistari
ambayo ameshaandika Wema Sepetu kwa ajili ya wimbo huo.
Mwambie wake ni mimi, na kwangu
moyoni atabaki ni yeye, tena mwambie bado silali kutwa nawaza penzi
langu… ila siku atakugundua kuwa mi ndo mwenyewe
Mpaka sasa hivi ni wimbo mmoja Wema alirekodi kwa kushirikiana na Snura ambapo Tunda Man alishiriki pia kuuandika
Hii hapa ni video siku ambayo Wema anarekodi sehemu kidogo ya wimbo wa kuhamasisha kumchangia Sajuki