MASTAA wawili wanaotamba katika filamu za Kibongo, Kajala
Masanja na Wema Isaac Sepetu hivi karibuni walifunga safari hadi Gereza
la Ukonga jijini Dar kwa ajili ya kumuona Johnson Nguza ‘Papii Kocha’
anayetumikia kifungo cha maisha gerezani humo.
Kajala Masanja na Wema Isaac Sepetu.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, mara baada ya mastaa hao kufika na
kuonana na Papii Kocha ambaye anatumikia kifungo cha maisha sambamba na
baba yake Nguza Viking ‘Babu Seya’ inadaiwa kuwa Papii aliangua kilio
cha nguvu.
“Nimewaona Kajala na Wema Gerezani Ukonga,wameenda
kumuona Papii Kocha. Sasa nimeamini kuwa Kajala amejifunza mengi
kutokana na kuwekwa mahabusu kipindi kile,” kilisema chanzo chetu kwa
sharti la kutotajwa jina lake gazetini.
Johnson Nguza ‘Papii Kocha’.
Baada ya kupata taarifa hizo Risasi Mchanganyiko liliwatafuta mastaa hao ili kutaka kujua undani wa safari yao hiyo.
Gazeti hili liliwapigia simu na kuzungumza na Kajala baada ya namba ya Wema kutokuwa hewani.
“Kweli mimi na Wema tulienda gerezani kumuona Papii ilikuwa ni safari
ya majonzi sana, Papii aliangua kilio sana alipotuona,” alisema kwa
kifupi Kajala na kukataa kusema kilichojiri zaidi.