NORA ACHOMOA ISHU YA KUBADILI DINI AOLEWE

 
MSANII wa filamu Bongo, Nuru Nassoro ‘Nora’ amefunguka kuwa japokuwa anampenda mpenzi wake wa sasa, Geofrey Kusila, hayupo tayari kubadilisha dini yake ya Kiislamu ili aolewe.

 
Akichonga na paparazi wetu hivi karibuni, Nora alisema endapo watafikia muafaka wa kuoana na mpenzi wake huyo, hawezi kubadili dini wala kufunga ndoa ya bomani kwa sababu anaipenda dini yake hivyo itabidi mwanaume amfuate.
“Siwezi kubadili dini na sitaki kufunga ndoa ya bomani, nataka ndoa yetu ibarikiwe na Mungu kwa sababu nampenda Geofrey ila hatuwezi kufunga ndoa bomani,” alisema Nora.

chanzo; http://www.globalpublishers.info.
back to top