JACK PATRICK , ***" NILIKURUPUKA KUOLEWA MAPEMA"*
MWANAMITINDO marufu Bongo, Jacqueline Patrick ‘Jack’ amesema alikurupuka
kuolewa na aliyekuwa mume wake, Abdulatif Fundikira ‘Tiff’ kwa kuwa
hakufanya tathmini ya kina kabla ya kufanya maamuzi.
Akizungumza na mwandishi wetu, Jack alisema laiti angekaa kwenye uchumba
kwa angalau muda wa miaka miwili kuchunguzana kabla ya kuoana mwaka
2011, asingeweza kufikia hatua ya ndoa kwani wangeshindwana tabia
mapema.
“Nilikosea, nikakurupuka kuolewa mapema bila kumchunguza
tabia mpenzi wangu, uhusiano wetu ulidumu miezi mitano tu kisha
tukafunga ndoa, lakini matokeo yake tabia hazikuendana na ndoa ikakosa
uhai ndani ya muda mfupi,” alisema Jack.