FEZA APONEA CHUPUCHUPU KUTOKA KWENYE JUMBA LA BIG BROTHER THE CHASE, ONEL OUT

 
 Homa iliyokuwa ikiwakabili watanzania kwamba huenda muwakilishi pekee kutoka Tanzania, Feza Kessy siku zake zimeisha kutoka kwenye jumba la Big Brother imepata tiba usiku huu ambapo muwakilishi huyo, amebaki bali mpenzi wake Oneal kutoka Botswana, ndio ametoka.

Oneal amekiri baada ya kutoka kwamba ni kutoka moyoni mwake, anampenda mshiriki huyo kutoka Tanzania na ana imani kwamba baada ya kutoka ndani ya jumba hilo, watakutana tena na kuendeleza walichokianza ndani ya jumba.

back to top