
STAA wa filamu na muziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohammed ‘Shilole’
ameingia matatani akidaiwa kuingia mitini na simu tatu za mkononi
alizoaminiwa nchini Afrika ya Kusini alikokwenda kufanya shoo.
Mfano wa aina ya simu anazo daiwa kuiba Shilole
Msanii huyo alikumbwa na kasheshe hilo Julai 19, 2013 nyumbani kwa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Sinza Mori, Dar.
Siku hiyo Diamond alikuwa akifuturisha na aliwaalika watu mbalimbali wakiwemo mastaa lakini nusura futuru iingie doa kufuatia zogo hilo.
ISHU ILIKUWAJE?
Ndugu wa Diamond aitwaye Majaliwa Majuto ‘Q Boy’ alidai ndiye mwenye simu hizo. Alisema miezi kadhaa iliyopita, Shilole alikwenda nchini humo kufanya shoo ya muziki. Wakati wa kuondoka alimpa simu tatu, Ipad, Samsung Galaxy na Blackberry ili akifika Bongo ampe Diamond lakini msanii huyo hakufanya hivyo.
“Alikuja
Sauzi kufanya shoo, wakati wa kuondoka nilimpa simu tatu amletee
Diamond lakini nashangaa hakufanya hivyo na mimi tangu nirudi Bongo
simpati, kila nikimpigia simu hapokei, leo ndiyo tumekutana hapa kwa
Diamond,” alilalama Q Boy.
DIAMOND ALIAMBIWA SIMU ANAZO SHILOLEAlisema awali akiwa nchini humo baada ya kumkabidhi mali hizo, alimpigia simu Diamond na kumtaarifu kuwa ‘mzigo’ anao Shilole, akashangaa staa huyo kujibu kwamba hajazipata wala hajamwona Shilole.