MSHAMBULIAJI GONZALO HIGUAIN MKAO WA KULA ARSENAL BAADA YA KUTHIBITISHA ANAONDOKA REAL MADRID MSIMU HUU

Mshambuliaji Gonzalo Higuain ameiweka mkao wa kula  Arsenal baada ya kudhibitisha kuwa msimu huu ataondoka kwenye klabu ya Real Madrid.
Arsene Wenger ambaye anataka kuborsha safu yake ya ushambuliaji,inafahamika kuwa anamzimikia mno mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Argentina.

Na baada ya kufunga katika ushindi wa Real Madrid wa 4-2 dhidi ya Osasuna Higuain alionesha nia yake ya kuondoka Bernabeu."Naondoka Real Madrid,uamuzi umekwisha afikiwa nafikiri ni wakati mwafaka na nina taka kubadilisha upepo",alisema.

Sijaamua nita kwenda wapi,lakini klabu tayari inafahamu nataka kuondoka.Ulikuwa uamuzi wangu .Mwisho wangu hapa.Nilitua hapa kwa paundi milioni 10 na ninaondoka kwa zaidi alesema Gonzalo.
back to top