WABUNGE WAANZA KUJIHAMI NA MILIPUKO YA MABOMU....WAMEOMBA ULINZI UIMARISHWE BUNGENI

MBUNGE  wa Jimbo la Simve kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Richard Ndasa amemuomba Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda kuhakikisha usalama wa Bunge unaimarishwa.
Ndasa aliyasema hayo wakati akichangia hoja katika Bajeti ya wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na kusema kuwa tukio la juzi Mjini Arusha kwa Bomu kurushwa katika sherehe za uzinduzi wa jingo la Kanisa Parokia ya Mtakatifu Joseph Mfanyakazi la Olasit mjini Arusha na kupelekea vifo vya watu wawili na wengine zaidi ya 50 kujeruhiwa vibaya.

“Mheshimiwa Spika, naomba usalama Bungeni uimarishwe na katika jingo la Bunge maana hofu ya kushambuliwa Bunge hili inaweza kutokea enbdapo ulinzi utakuwa hafifu,” alisema Ndasa.

Ndasa alitolea mfano eneo la nyuma la Bunge hilo kuwa halina ulinzi wa kutosha hivyo ni rahisi mtu kusogea jirani na kufanya uhalifu nakuleta madhara makubwa kwa taifa.

Wabunge leo wanaendelea kuchangia Hotuba ya Wizara ya Mambo ya Ndani huku kila anaesimama akilaani tukio hilo la Arusha.
back to top