VIDEO YA CHID BENZ ALIPOCHEZEA KICHAPO PALE MAISHA CLUB

 Jumapili hii kwenye ukumbi wa New Maisha Club, kulitokea ugomvi kati ya rapper Chidi Benz na Kalapina aliyekuwa na show yake pamoja na Kikosi cha Mizinga. 

Tukio lilitokea baada ya Chidi Benz kupanda ghafla kwenye stage na kumnyang’anya kipaza MC wa show hiyo wakati Nikki Mbishi alipokuwa kwenye stage. 

Baada ya kupanda juu, Chidi aliyekuwa amelewa alianza kuwaongelesha na kuwaimbia mashabiki waliokuwa wakimshangilia. 


“Naomba niongee kitu kimoja ambacho ninyi watu woote ambao mpo humu ndani mtasikiliza, au vipi, nimeingia na beibe beibe, nimeingia VIP halafu nimemuona Nikki Mbishi anachana hapa stage, Nikki njoo njoo Nikki njoo, sijui show ya nani kwasababu yako wewe nimekuona nilikuwa paleeee, nimepita nimekuja hapa nimekuona mdogo wangu, sasa nini sasa, piga keleleeee,” alisikika akisema Chidi huku watu wakimshangilia na baadaye microphone kuzimwa. 
 
Baadaye Kalapina alipanda kwenye stage na kuchukua microphone, “Oii ambaye hahusiki na show ashuke,” alisema Kalapina na kumfuata Chidi kisha kumpiga na kumwangusha chini. “Ninyi mnamwachia mtoto m*** apande kwenye stage,” alisema Kalapina wakati huo Chidi Benz aliyekuwa anataka kurudi tena kwenye stage kupigana akiwa ameshikiliwa na watu wa ulinzi.

VIDEO : CHID BENZ ACHEZEA KICHAPO KWA MARA NYINGINE  TOKA  KWA  KALAPINA
back to top