Meneja wa Manchester
City Roberto Mancini anaamini kuwa kurejea kwa Jose Mourinho katika klabu ya Chelsea kutaongeza uchangamfu wa ligi kuu ya
soka nchini England Premier League na kuongeza kuwa kutaifanya klabu hiyo kuwa
klabu ya tatu katika haraki za kuwani taji msimu ujao.
Baada ya
kuwa katika msimu wa shida kwa meneja wa huyo mwenye umri wa miaka 50 sasa kuna
tetesi za kutaka kurejea katika klabu yake hiyo hya zamani na kuihama Real
Madrid huku tayari zikiwepo habari za chini chini kuwa tayari ameshakubaliana mambo
ya msingi na klabu yake hiyo ya zamani baada ya miaka 6 kupita tangu aihame
Mancini
amenukuliwa na Gazetta Extra Time akisema
"itakuwa
ni uchangamfu mpya wa ligi na Chelsea itakuwa katika vita ya kuwania taji,"
Chuck Blazer apigwa stop kazi ya
utendaji wa FIFA na CONCACAF
Baada ya
kutuhumiwa kufanya makosa ya kimaadili ya utendaji ndani ya shirikisho la soka
duniani FIFA, mtendaji mkuu wa shirikisho la soka la Marekani ya kaskazini,
kati na Caribbean CONCACAF, Chuck Blazer ameadhibiwa.
FIFA imetangaza
adhabu hiyo jana kwamba Blazer amefungiwa kwa kipindi cha siku 90.
Blzer mwenye
umri wa miaka 68 ametuhumiwa kuchukua zaidi ya dolari za kimarekani milioni $20
kutoka CONCACAF wakati wa kipindi chake cha uongozi kama katibu mkuu.
Taarifa ya
FIFA imesomeka kuwa
"mwenyekiti
wa kitengo cha kisheria na maadili cha FIFA Hans-Joachim Eckert, ameamua
kumfungia mjumbe wa kamati ya utendaji wa FIFA Chuck Blazer kutokushughulika na
shughuli zozote za soka kuanzia ngazi ya kitaifa na kimataifa kwa kipindi
kisicho pungua siku 90.
"Mamuzi
hayo yanafuatia ombi la kaimu mwenyekiti wa kitengo cha uchunguzi wa kimaadili Robert
Torres, kutokana na kuonekana kwa uvunjifu mkubwa wa kimaadili uliofanywa na Chuck
Blazer. "
Sunil Gulati
ameteuliwa kushika nafasi ya Blazer katika kamati na ameahidi kuwa muwazi
katika yote ya kibadhirifu yaliyotokea katika kipindi cha uongozi wa CONCACAF chini
ya Jack Warner na Blazer.
Blazer anatarajiwa
kujiuzulu mwenyewe kutoka katika uongozi wa FIFA May 30.
Balotelli kupigwa faini
Mtendaji
mkuu wa AC Milan Adriano Galliani amethibtisha kuwa Mario Balotelli atakumbana
na adhabu baada ya kushangiliwa kwa kuvua jezi katika mchezo wa jumamosi dhidi
ya Torino ukiwa ni mchezo wa ligi kuu ya soka nchini Italia ambapo Balotelli
alivua jezi yake baada ya kufunga goli pekee la ushindi.
Hata hivyo Galliani
ameonyeshwa kufurahishwa na kasi ya ufungaji mabao ya Balotelli mwenye umri wa
miaka 22 ambapo sasa ana magoli 9 kati ya michezo 10 ya Serie A aliyocheza.
Amenukuliwa akisema
"kwa
kuwa anafunga magoli zaidi kuvua jezi hilo si tatizo lakini ieleweke kuwa kuvua
jezi haikubaliki "
Tello: Sijafikia uwezo wa Henry bado.
Cristian
Tello amesema kuwa bado hajafikia uwezo wa Thierry Henri na kwamba bado ana
safari ndefu ya kufikia na kulinganishwa na mshambuliaji huyo wa zamani wa Barcelona.
Tello mwenye
umri wa miaka 21 amekuwa akilinganishwa na nyota huyo mqwenye heshima kubwa na
alama muhimu katika klabu ya Arsenal kufuatia aina yake ya ushambuliaji katika
sehemu ya ushanbuliaji wa kushoto ya Blaugrana ambapo mwenyewe amekataa na kuweka
wazi kuwa bado kufikia kiwango cha mfaransa huyo.
Amenukuliwa na
Barca TV akisema
"bado
nina safari ya kufikia soka na magoli yake "
Hata hivyo Tello
alienda mbali zaidi na kuzungumzia umuhimu wa mshambuliaji Lionel Messi ndani
ya Barcelona ambapo amesisistiza kuwa kukosekana kwake kulionyesha wazi umuhimu
wake katika mchezo wa pili wa marudiano dhidi ya Bayern Munich katika ligi ya
mabingwa Ulaya.
Wapinzani wa soka la Moroccan wakutanishwa
kombe la shirikisho hatu ya 16
Timu mbili
za Moroccan FUS Rabat na FAR Rabat zimekutanishwa katika hatua ya 16 bora ya
michuano ya shirikisho hatua ya 16 michezo ya play-off .
Timu hizo
mbili ambazo zinatumia uwanja mmoja wa Prince Moulay Abdellah watakutana kusaka
nafasi ya kuingia hatua ya makundi ikiwa ni michuano ya pili mikubwa ya ngazi
ya vilabu barani Afrika.
Hatua hii ni
ya michezo miwili ya nyumbani na ugenini ambapo timu 8 zilizoshindwa kutoka
michuano ya klabu bingwa Afrika zinaunganishwa katika hatua 16 bora ya michuano
yua shirikisho kusaka nafasi ya kuingia hatua ya makundi.
Michezo ya
kwanza itapigwa May 15 mpaka 17 huku michezo ya marudiano ikitarajiwa kuchezwa
May 31 na June 2.
Pamoja na
mchezo huo wa timu ndugu toka Morocco pia TP Mazembe baada ya kushindwa na
Orando pirates ya Afrika kusini sasa wamepngwa kucheza na Liga Muculmana ya
Mozambique.
Muculmana ambao
katika mchezo wa hatua ilipita waliwapeleka puta Wydad Casablanca ambao
walipona kwa sheria ya faida ya bao la ugenini sasa wanakumbana na kigogo
kingine Mazembe.
Wamisri wengine
wa Enppi wamepangwa kukutana na St George ya Ethiopia ambao waliwapa shida Zamalek
katika mchezo wa hatua iliyopita ya klabu bingwa Afrika.
CA Bizertin
ya Tunisia iliyotolewa na mabingwa Al Ahly watakuwa na kazi kubwa kuwafungasha
virago Ismaili ya Misri.
Washindi 8 wa michezo hiyo ya play-off watatengeneza makundi mawili ya timu nne
ambayo washindi wa kwanza na wa pili watasonga mbele kwa nusu fainali.
Droo hii hapa.
Stade Malien
(Mali) v Lydia LB Academic (Burundi)
Enugu Rangers
(Nigeria) v CS Sfaxien (Tunisia)
FUS Rabat
(Morocco) v FAR Rabat (Morocco)
CA Bizertin
(Tunisia) v Ismaili (Egypt)
Entente
Setif (Algeria) v US Bitam (Gabon)
JSM Bejaia
(Algeria) v Etoile du Sahel (Tunisia)
TP Mazembe
(DR Congo) v Liga Maculmana (Mozambique)
St George
(Ethiopia) v Enppi ( Egypt)