Gazeti la chama tawala cha china, People’s Daily ambalo limezoea kuwa
kitovu cha kusambasa habari, sasa limejikuta likiwa habari baada ya watu
wenye fikra za kitukutu kuona jengo jipya la gazeti hilo limefanana na
nyeti za kiume.
Jengo hilo lenye urefu wa mita 150, hivi sasa bado linaendelea
kujengwa jijini Beijing. Kutokana na muundo huo usiokua wa kawaida,
picha za kibunifu zikaanza kuibuka katika website ambayo ni kama
“Twitter ya China,” inayoitwa Sina Weibo.
Watu wengi wameeleza kuwa kwa kutumia ubunifu kidogo tu wa
photoshopping, unaweza kuambatanisha picha ya jengo hilo, ambalo raia
wamelipa nickname “Giant Pen*s” au “Uume mkubwa,” katikati ya “miguu” ya
jengo lingine maarufu nchini humo ambalo ni makao makuu ya kituo cha TV
cha China Central Television (CCTV,) linalojulikana kwa nickname ya
“Big Und*rpants” building au Jengo la Chupi Kubwa.
Habari za utani huo zilifikia wakubwa nchini humo ambao walikerwa na
kuamua kuwaharibia watu raha zao kwa kuamuru website ya Sino Weibo
ku-block search zote zinazotafuta picha au habari za jengo hilo.
Kwa
sasa Wachina wakitafuta jengo hilo, wanakutana na ujumbe “kuendana na
sheria, kanuni na sera husika, matokeo ya utafutaji wako (search
results) hayawezi kuonyeshwa."
Mwandishi wa Reuters, Anita Li amesema “hii inaonyesha frustrations
miongoni mwa vijana watumiaji wa internet nchini China, na pia
inaonyesha ni kiasi gani “wakubwa” wako sensitive kwa hata vitu vidogo
vya kipuuzi online.”
Laivu.com