Wakihojiwa kwa nyakati tofauti, baadhi ya wasichana wanaojishughukisha na biashara hiyo wameelezea changamoto mbalimbali wanazokutana nazo katika kazi hiyo hususani nyakati za usiku.
Wakizungumzia adha wanazokutana nazo Wasichana hao wamesema kuwa licha ya kukabiliwa hali ngumu ya maisha iliyopelekea kuingia katika biashara hiyo, bado wamekuwa wakikutana na matukio mabaya ikiwemo kukamatwa na kuingiliwa kinguvu na baadhi ya watu wanaojitambulisha kwao kuwa ni askari wa Polisi jamii.
Mbali na hilo Wasichana hao wamesema hali ngumu ya Maisha imekuwa ikiwalazimu kufanya mapenzi kinyume na maumbile wanapokuwa kwenye Hedhi, pasipo kujali hatari ya kukumbwa na maradhi yoyote.
Hivi karibuni Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni lilitangaza mpango wa kuwaondoa wasichana wamaojishughulisha na Biashara ya ngono mitaani na kuwashtaki kwa mujibu wa Sheria ya makosa ya uvunjifu amani na ukiukwaji wa maadili.
Wakizungumza baadhi ya wadau kutoka mashirika na Taasisi mbalimbali za kutetea haki za Binadamu nchini, ambapo kituo cha Sheria na haki za Binadamu pamoja na taasisi ya kutetea haki za Binadamu ya Chuo Kikuu cha Tumaini, kimesema kuwa kitendo cha kuwakamata wasichana hao hakiwezi kuwa suluhisho la kutokomeza Biashara ya ngono nchini.
Eneo la MANZESE Uwanja wa Fisi ni miongoni mwa Maeneo ambayo Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es salaam limeliainisha kuwa limekuwa likikithiri kwa Biashara hiyo
Credit: Cloudsfm