Ni suala la kawaida kuona watoto wamejipanga kando ya barabara wakiomba wasamaria wema.
Wapo ambao wako peke yao wakifanya kazi hizo,
wengine wanafanya kazi hiyo wakiwa na wazazi wao; wazazi hukaa kando
kusubiri kuwanyang’anya kile ambacho watoto wanaomba kutoka kwa
wasamaria wema.
“Nimetoka Dodoma, huu ni mwaka wa tatu, niko na
mama na bibi, wao mara nyingi huwa wanakaa pembeni ya barabara, sisi
watoto ambao ni wanne ndio tunaoingia katikati ya barabara kuomba hasa
wakati magari yanaposimama,”anasema, John Francis (sio jina lake halisi)
mwenye umri wa miaka 12 akiwa maeneo ya Faya, Kariakoo jijini Dar es
Salaam.
Watoto wengi wa mitaani wanaonekana kuteswa mno
hasa usiku kwa kubakwa na kulawitiwa na hata kupigwa pale wanapokataa
kile ambacho walio wakubwa kwao wanataka ikiwemo kufanyishwa vitendo vya
ngono au kutoa fedha walizoomba au walizopata kutokana na kazi
mbalimbali zikiwemo kuosha magari.
Huenda ndiyo ‘majambazi’ wa kesho
Hata hivyo kinachoonekana ni kwamba baadhi ya watoto hawa huenda wakawa ni majambazi,kwani kwa mujibu wa Mwanasaikolojia, Modesta Kimonga kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma, kitaalamu mtu ambaye anaishi katika hali fulani ngumu ikiwamo kiuchumi, ni rahisi kwake kushawishiwa kufanya lolote.

Wasio na jamaa wako hatarini zaidi
“Kuna kijana aliwahi kutaka kunilawiti, nilikataa, nilimwambia mama alimtukana na kutaka kumpiga.Wanaobakwa na kulawitiwa sana ni wale ambao hawana watu wa kuwasaidia, unakuta wengine wametoka mikoani, wapo hapa Dar es Salaam, hawana ndugu wala jamaa,” anasema Francis.

Usiku ni jehanamu
Katika utafiti ambao mwandishi amefanya katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam, yakiwamo Ubungo katika makutano ya barabara ya Mandela, Morogoro na Sam Nujoma, Kariakoo, Posta, Kinondoni, Magomeni, Buguruni, Kawe na Mwenge ambako kunaonekana kuwa na watoto wengi wa mitaani hasa kutokana na kuwa na shughuli nyingi za mbalimbali za kijamii, usiku ni wakati wa hatari zaidi kwa watoto, kwani ndipo huwa wanafanyiwa kila aina ya ukatili, huku wakiwa hawana wa kuwasaidia.

Katika eneo la Magomeni, makutano ya barabara
itokayo Kinondoni kwenda Jangwani, jijini Dar es Salaam, kuna watoto
ambao wanaosha magari, utafiti unaonyesha baadhi yao wamekuwa
wakiingiliwa usiku na baadhi ya watoto wa mitaani walio wakubwa au watu
wengine ambao sio ombaomba kwa ahadi za kuwasaidia waondokane na maisha
duni yanayowasumbua.
“Ni kweli nimewahi kuingiliwa, siyo kwamba
nilipenda, nakumbuka siku hiyo mvua ilinyesha sikuwa na pa kulala, kwani
mimi na watoto wenzangu huwa tunalala nje. Kuna jamaa mmoja mtu mzima
ambaye naye huwa tunasafisha naye magari na shughuli zingine za mitaani,
ana chumba aliniingilia kwa nguvu, alianza polepole, hatimaye
alifanikiwa kuniingilia, nililia sana, sikuwa na la kufanya. Baada ya
hapo akawa karibu nami kunisaidia mambo mengi yakiwemo kuninunulia
chakula ninapokuwa sina fedha,” anasema mtoto mmoja katika eneo la
makutano hayo (jina limehifadhiwa).
Katika eneo hilo la makutano ya barabara ya kutoka
Kinondoni kwenda Jangwani, kuna mtoto mwingine ambaye muda mwingi huwa
anasinzia kumaanisha kwamba huwa amekuwa amelewa, ana umri wa miaka 14,
anasisitiza “Ni kweli kuna watoto wengi wanaingiliwa kinyume na maumbile
hasa kama mtoto mwenyewe anapenda kula vizuri,” anasema mtoto huyo,
aliyeingia jijini akitokea Mwanza kwa kumhonga fedha kidogo kondakta wa
basi moja linalotoka Mwanza kuja Dar es Salaam ili kuja kujaribu maisha
jijini, kwani kule Mwanza anasema japo wazazi wake wako hai, hawana
uwezo.
Katika eneo la Kawe, kwenye bonde ambalo ni mpaka
wa Kawe na Mbezi, kuna kundi la watoto linaloitwa Mbwakoko, kwa maana
kuwa kwa haraka unaweza kufikiri ni watoto wazembe hivi, lakini
ukikaribiana nao usiku utakiona cha moto.
Wana umaarufu katika eneo hilo, kwa matendo yao,
kuna wakati wenyeji wanasema huwalazimisha wanaopita eneo hilo kutoa
fedha, wanapokataa huwadhuru au hata kuwatishia kwa maneno makali.