
Shule hiyo ya mchepuo wa sayansi ambayo ilianzishwa mwaka 1950, imeingia katika migogoro baina ya uongozi wa shule hiyo na wafanyakazi na baadhi ya wanafunzi.
Wanafunzi 10 walisimamishwa hivi karibuni 10 kutokana na utovu wa nidhamu, hatima yao inasubiri kikao cha bodi ya shule Aprili 17, mwaka huu.
Wakati wanafunzi hao wakiwa wamesimamishwa, walimu watatu
wamepewa barua za uhamisho ikitajwa kama sehemu ya kuboresha ikama ya
ualimu shuleni hapo.
Kaimu mkuu wa shule hiyo, Twaha Mruma alimweleza Kaimu Mkuu wa
Wilaya ya Iringa, Gerald Guninita aliyefika shuleni hapo jana kujionea
kiwango cha uharibifu huo kuwa, matukio ya kuchomwa moto majengo hayo
ni hujuma. Alisema matukio hayo yalianza Mwezi Aprili 4, mwaka huu na
yamefanywa kwa siku tatu mfulululizo