Kaimu Mkurugenzi wa Biashara, Bi. Mwanamvua Ngocho, akizungumuza
na wageni waalikwa, abiria waliosafiri na ndege la shirika hilo, pamoja
na maofisa wa uwanja wa ndege la Mtwara (hawapo pichani) wakati wa
uzinduzi wa safari za ndege za Shirila la Ndege la Tanzania (ATCL)
mkoani Mtwara , mara tu baada ya kutua ndege hiyo uwanjani hapo mwishoni
mwa wiki.

Meya
wa Mtwara Mikindani, Selemani Mtalika Shilingi ambaye alikuwa mgeni
rasmi wakati wa uzinduzi wa safari za ndege za Shirila la Ndege la
Tanzania (ATCL) mkoani Mtwara, akizungumuza na wageni waalikwa, abiria
waliosafiri na ndege la shirika hilo, pamoja na maofisa wa uwanja wa
ndege la Mtwara (hawapo pichani) mara tu baada ya kutua ndege hiyo
uwanjani hapo mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Kaimu
Mkurugenzi wa Biashara, Bi. Mwanamvua Ngocho na kulia ni Meneja
Rasilimali watu na Utawala, Bi. Halima Nabalang’anya. Picha na mwandishi
wetu.

Baadhi
ya abiria waliopanda dege ya Shirika la ndege la Tanzania (ATCL),
wakitembea kuelekea katika chumba cha kupumzikia abirai, wakati wa
uzinduzi wa safari za ndege za shirila hilo mkoani Mtwara iliyofanyika
mwishoni mwa wiki.
====== ====== ========
Safari za ndege ya ATCL kwenda Mtwara zaanza
Na Mwandishi Wetu
SHIRIKA
la Ndege la Air Tanzania (ATCL) mwishoni mwa wiki lilizindua upya
safari zake za moja kwa moja za Dar es Salaam-Mtwara na kuahidi kuongeza
idadi ya safari hizo na kutoza nauli nafuu.
Akizungumza
baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Mtwara, Kaimu Mkurugenzi wa
Biashara, Bi. Mwanamvua Ngocho alisema kuwa kurejeshwa kwa huduma za
usafiri wa anga na shirika hilo la taifa mjini Mtwara ni chachu ya
mapinduzi makubwa katika usafiri wa anga mjini hapo kwa kuhakikisha kuwa
abiria wanapata huduma bora na za kiushindani.
"Nataka
kuwahakikishia wakazi wa Mtwara kwamba ndege yao ya taifa imekuja
kuwahudumia watu wa mkoa huu. Kwa kuanzia, tutaruka Mtwara mara nne
katika wiki; ikiwa ni siku za Jumatatu, Jumatano, Ijumaa na Jumapili,
lakini tutaendelea kufanya marekebisho ya safari kutegemeana na
mahitaji. Abiria watarajie ATCL kuwapatia huduma ambazo ni salama na za
gharama nafuu, "alisema.
Mwanamvua
alieleza kuwa shirika hilo litatoza shilingi 199,000 / - kwa tiketi ya
kwenda na kurudi, na kuahidi kuwa shirika hilo litafanyia kazi suala la
kupunguza gharama za usafiri zaidi ili kuwawezesha wasafiri wanaoenda na
kutoka Mtwara kuona faida za kutumia usafiri wa anga.
Kwa
upande wake, Meya wa Mtwara Mikindani, Selemani Mtalika Shilingi ambaye
alikuwa mgeni rasmi, alisema baada ya ndege ya taifa kurejesha huduma
zake mkoani Mtwara, wakati wa shirika moja la ndege kutawala utoaji
huduma mkoani hapo na kulazimisha abiria kulipa nauli za juu, sasa
umekwisha.
“Ninafuraha
kuona shirika la ndege la taifa likiwa limerejesha huduma zake mkoani
Mtwara. Kwa muda mrefu sasa usafiri wa anga hapa Mtwara imekuwa
ikitawaliwa na shirika moja tu la ndege. Ukweli ni kwamba, pasikuwepo na
ushindani, suala la bei mara nyingi ni changamoto kwa walaji/wateja.
Abiria wa kwenda na kutoka Mtwara wamekuwa wakilipa nauli za juu. Ila
kwa kuwa tuna ATCL sasa na Kaimu Mgurugenzi wa Biashara ametuakikishia,
wakazi wa Mtwara na wageni wetu watapata fursa ya kufurahia usafiri wa
anga ulio salama na wa gharama nafuu,” alisema Shilingi.
Meya
huyo alisema kuwa idadi ya abiria wanaokwenda Mtwara imekuwa
ikiongezeka sana katika siku za karibuni, kwa sababu Mtwara imekuwa na
sura ya kibiashara baada ya ugunduzi wa kiasi kikubwa cha gesi asilia na
kuwa mkoa unaozalishaji zao la korosho kwa wingi hapa nchini.
“Wawekezaji
wengi wanaendelea kumiminika katika mkoa wetu, na hivi karibuni Mtwara
itakuwa na muonekano tofauti kabisa. Ushawishi huu wa kuwekeza mkoani
Mtwara umeongeza idadi ya abiria wanaosafiri na ndege. Nina uhakika ATCL
itaona ongezeko la abiria mapema na kulifanya shirika kuongeza idadi ya
safari zake mapema,” alisema.
Shirika
hilo litatumia ndege yake aina ya Dash 8-300 yenye uwezo wa kubeba
abiria 50, wakati huu wa mwanzoni, lakini uongozi umebainisha kuwa pale
idadi ya abiria itakapoongezeka kuzidi uwezo wa Dash 8, watatumia ndege
yao aina ya Boeing.
Urejeshwaji
wa safari za Mtwara umekuja ikiwa ni mwezi mmoja tu baada ya shirika
hilo pia kurejesha safari za Kigoma baada ukarabati wa uwanja wa ndege
wa Kigoma kumalizika.