NIMEZOEA MAISHA YA KIBACHELA, ASEMA CHUCU HANS!

STAA ambaye hivi sasa anafanya vizuri kwenye tasnia ya filamu Bongo, Chuchu Hans, amesema licha ya kuolewa lakini amezoea kuishi maisha ya ubachela kwa muda mrefu.  
Akizungumza na Risasi Jumamosi, Chuchu alibainisha kuwa ni kipindi kifupi sana alichoishi na mumewe ambaye alikuwa mtangazaji wa Televisheni ya Channel Ten, Frank  Mtao, ambaye sasa yupo Sidney, Australia kikazi.

“Unajua mimi nimeshazoea kabisa maisha ya ubachela na hata kuna wakati najisahau kama niliolewa kwa maana nimeshakaa peke yangu muda mrefu sana  lakini nashukuru Mungu nina marafiki wengi wanaonipa kampani hivyo upweke unaondoka,” alisema Chuchu.
back to top