Chama
cha Kutetea Abiria Tanzania (CHAKUA) kimesema
kinaiburuza kortini Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini
na Nchikavu (SUMATRA), kwa madai kuwa hakikushirikishwa
kwenye mchakato wa kuongeza nauli za abiria.
kinaiburuza kortini Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini
na Nchikavu (SUMATRA), kwa madai kuwa hakikushirikishwa
kwenye mchakato wa kuongeza nauli za abiria.
Aidha, CHAKUA kimeitaka serikali kuuwajibisha uongozi wa juu wa SUMATRA kwa kuifuta na kuunda upya kwa madai kwamba imeshindwa kusimamia maslahi ya wananchi wanyonge.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mshauri wa chama
hicho, Wilson Mashaka, alisema tangazo la kupandisha nauli halikujengwa
kwa dhana ya ushirikishwaji, kwani vikao vilivyofanyika kati ya
Septemba na Novemba, 2012, vilifanyika kwa kuwashirikisha wamiliki wa
mabasi lakini wadau muhimu kama CHAKUA hawakushirikishwa.