Hakuna lugha nyepesi unayoweza kuzungumza zaidi ya kusema haya ni maajabu ya mwaka 2013, kwani familia ya Masoud Kassim wa Karakata Ukonga Dar imejikuta ikiingia kwenye mgogoro wa kisheria baada ya kuamua kumfanyia ‘kitchen party’ mtoto wao wa miaka 13 aitwaye Rafia Masoud, tayari kwa ndoa.

Tukio hilo la kusikitisha na kuhuzunisha limetokea Jumatano ya wiki iliyopita ambapo Gpl ilikuta Rafia akiwa katika sherehe hizo huku ndoa yake ikitarajiwa kufungwa leo Februari 2.
