
Wanafunzi wakiwa na mabango leo mjini dodoma.
ZAIDI ya wanafunzi 4000 wa Chuo Kikuu cha St. John’s kilichopo mjini DODOMA
wameandamana wakililalamikia Jeshi la Polisi Nchini kwa kushindwa
kuthibiti vitendo vya matukio ya ubakaji na kulawitiwa yanayofanyika
chuoni hapo.
Wanafunzi hao ambao waliandamana umbali wa kilomita tatu leo kutoka chuo kilipo
na kuishia viwanja vya Mwalimu Nyerere walidai wanalenga kufikisha
ujumbe kwa jamii kutambua vitendo vya kikatili vinavyofanyika chuoni
hapo.
Maandamano hayo ambayo yalikuwa yakisindikizwa na
Polisi wa kikosi cha kutuliza ghasia, yalipita katika mitaa mbalimbali ya Manispaa ya Dodoma.
Waandamanaji hao ambao mbali na kuimba nyimbo za kulilaumu Jeshi la Polisi kwa kushindwa kuthibiti vitendo hivyo, pia mabango waliyokuwa wamebeba yalikuwa yakililaumu jeshi hilo.

Askari jeshi la polisi wakijariobu kuwazuia wanafunzi leo mjini dodoma