Mwenyekiti wa POAC, Kabwe Zitto
Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma (POAC), imeliagiza Shirika la
Utangazaji (TBC) kuacha kurusha matangazo ya biashara ili kuweka uwanja
sawa na televisheni pamoja na radio binafsi.
Mwenyekiti wa POAC, Kabwe Zitto, alitoa maelekezo hayo jana wakati kamati yake ilipokutana na TBC pamoja na Kituo cha Uwekezaji (TIC) na kuangalia mkataba baina ya shirika hilo na kampuni ya Star Media.
Alisema kitendo cha TBC kuruhusiwa kurusha matangazo ya biashara kinaondoa ushindani baina yake na vyombo vingine vya habari vya binafsi.
Badala yake alisema kamati yake inapendekeza kwamba kuanzia Julai Mosi mwaka huu, TBC iwe inapewa Sh. 1,000 ya malipo ya kila king’amuzi.
“Tumependekeza kuwa TBC ni lazima iendeshwe na umma kwa sababu ni shirika la umma, hivyo linapaswa kutoa huduma siyo kufanya biashara, lengo ni kuondoa ushindani usio wa haki baina yake na vyombo vingine vya habari. Katika kila malipo ya king’amuzi ya kila mwezi, Sh. 1,000 iende TBC kwa ajili ya kuiendesha na isichukue matangazo ya biashara…TBC inaendeshwa na fedha za walipakodi, haiwezi kushindana na hao hao walipakodi,” alisema Zitto.
Alisema mapendekezo hayo yanalenga kuweka uwanja sawa kati ya vyombo vinavyoendeshwa na umma na vile vya binafsi.
Aliongeza kuwa maelekezo ya kamati yake yataanza kutekelezwa rasmi Julai Mosi mwaka huu “kwa hiyo basi TBC haitachukua matangazo ya biashara, kwa sababu inaendeshwa na umma…tukiwaruhusu wachukue matangazo ya biashara ni kwamba watakuwa wanayaonea makampuni binafsi katika biashara hiyo.”
Zitto alisema kwa maelekezo hayo, TBC itatoa huduma na itaendeshwa na kila mwananchi mwenye king’amuzi kwa kuwa Sh. 1,000 ya malipo ya mwezi itakatwa kwa ajili ya kuliendesha shirika hilo. “Tumeiambia TBC wawajulishe pia kamati ya Jenista Mhagama (Maendeleo ya Jamii) ili mapendekezo haya yaingizwe kwenye bajeti mwaka huu.”