DAYNA NYANGE KUVUKA MIPAKA YA BONGO KUFANYA WIMBO NA CINDY SANYU

 
Dayna Nyange.
Mwanamuziki  maarufu  nchini  Tanzania  mwanadada  Dayna  Nyange  mkali  wao,  amedhamilia  kuvuka  boda  na  kuonesha  dhamira  yake  ya  kufanya Collabo   na  wanamuziki  tok  nje.
   
Akizungumza  na Kajunason Blog kwa njia ya simu akiwa mjini  Morogoro, Dayna  alisema  kwa  sasa yuko katika  mpango  wa  mwisho  wa  kufanya wimbo  na  mdada anayetamba  nchini   Uganda  na  Africa  Mashariki anayefahamika  kwa  jina  la  Cindy.

    
''Nina  mpango  wa  kufanya  nyimbo  na  wasanii  tofauti wa  kibongo  na nje, lakini  kwa  sasa  nipo  katika  mkakati  wa  kufanya  wimbo  na  mdada  toka  Uganda  anayefahamika  kwa  jina  la  Cindy  ambaye  naamini  tunafanana  kwa  kiasi  kikubwa  sana''.  Amesema  Dayna.
 
Cindy.
back to top