Chadema: CC haikuwa na ajenda ya mpasuko ya


 Dk. Slaa
 Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa
Kamati  Kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), imesema suala la kuwepo mpasuko ndani ya chama hicho halikufika mezani kwake kwa  kuwa halikuwemo katika ajenda zilizotakiwa kujadiliwa na kutolewa maamuzi.

Habari za uhakika kutoka ndani ya kikao cha Kamati Kuu jana zilisema hapakuwa na mpango wowote wa kumjadili mtu yoyote na kwamba masuala yaliyozungumziwa ni pamoja na kuishinikiza serikali ili ikomeshwe mauaji yanayofanywa na Polisi dhidi ya raia.
Chanzo cha habari kililiambia NIPASHE kwamba baadhi ya taarifa zilizoandikwa jana na baadhi ya vyombo vya habari hazikuwa na ukweli.
“Baadhi ya mambo muhimu yaliyojadiliwa ni kuhusu namna ambavyo Chadema kuanzia mwakani kitaweza kuishinikiza serikali kupitia M4C ili ikomeshe mauaji na siyo kukutana kwa ajili ya kujadili watu,” kilieleza.
Kuhusu madai ya Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), ,kushinikiza Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa, chazo hicho kilisema: “Hizo zilikuwa ni taarifa za kutunga na kutokana na hali hiyo, hazikufika hata mezani kwa ajili ya kujadiliwa na Kamati Kuu.”
Aidha, Kamati Kuu ilipokea na kujadili barua waliyojibiwa na Rais Jakaya Kikwete ambayo alionyesha kukubali kushughulikia mauaji ya raia yanayofanywa na polisi. Kikao hicho kilichoanza juzi kilimazika jana jioni.
back to top