Ilie
kesi iliyokuwa inamuandama mfanyakazi wa kampuni ya usambaji filamu
nchi ya Steps Entertainment Ltd Selles Mapunda ya kutuhumiwa kumbaka
msanii mchanga aliyetajwa kwa jina moja la Nance sasa imefutiwa mbali na
Polisi Kituo cha Oysterbay kabla haijapelekwa mahakamani kwa madai
haikuwa na vielelezo vya kutosha toka kwa mshitaka.
Hata hivyo akiongea na Xdeejayz muda mfupi baada ya kesi hiyo kufutwa Mapunda alisema " Namshukuru Mungu hii kesi haikuwa na ukweli wowote lakini sala zangu kwa Muumba zimejibu na sasa niko huru ila nimesamehe kila kitu hata huyu bint pia nimemsamehe zaidi nashukuru wapelelezi wa kesi hii ambao wametenda hali" Alisema Mapunda
Hata hivyo bint huyo anaedaiwa kubakwa nae aliiambia Xdeejayz kuwa alishamuachia Mungu tangu mwaka jana na alishamsamehe Mapunda kwa yote aliyomfanyia hivyo anamchukulia Mapunda kama msanii mwenzake na kakaake hivyo hana kinyongo nae" Alisema dada huyo aliyetambulika kwa jina la Nance.