ROSE NDAUKA AZIDI KULILIA NDOA

STAA wa filamu za Kibongo, Rose Ndauka amezidi kulilia ndoa ambapo sasa ameonesha shauku ya kufunga hata ndoa ya mkeka ili kukata kiu yake ambayo amekuwa nayo kwa muda mrefu.

 
Staa wa filamu za Kibongo, Rose Ndauka.
Rose aliyejifungua hivi karibuni huku baba wa mtoto akijulikana kwa jina moja la Malick alisema hayo hivi karibuni nyumbani kwake Magomeni, Dar, ambako alikutana na mwandishi wetu aliyetaka kujua ndoa ya msanii huyo itafungwa lini?
“Nimeshasubiri sana,  nimejiandaa kwa kila kitu hata upande wa dini niko tayari kwenda sambamba na mume wangu mtarajiwa, naamini siku chache zijazo nitaolewa,” alisema Rose ambaye uchumba wake umekuwa ukifunikwa na sintofahamu kibao.
Rose aliongeza kuwa siku atakayofunga ndoa furaha yake itakuwa mara dufu kwa sababu tayari ana ‘baby’.
back to top