Mtangazaji Penniel Mungilwa ‘Penny’.
Penny alisema hayo hivi karibuni jijini Dar wakati akizungumza na
gazeti hili lililotaka kujua anazungumziaje tuzo saba za Kilimanjaro
alizojizolea Diamond ambapo majibu yaliyopatikana yalikuwa:
“Wanaotakiwa kuzungumzia hili ni mkewe na ndugu zake, mimi sitaki.”
Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Alipoulizwa mke wa Diamond ni nani alisema: “Mnamjua” na kuicha
historia ikibaki kuwa Penny na msanii huyo waliwahi kuwa katika mapenzi
mazito ya njiwa kabla ya kumwagana na mwanamuziki huyo kumrudia mpenzi
wake wa zamani, Wema Sepetu, ambaye mwenyewe anapenda aitwe mke
mtarajiwa. Hahahaha!