Labda
ingekua ya msanii wa Tanzania, Kenya, Uganda au Rwanda hii video
ingekua imeshafungiwa kwenye nchi anayotoka kama ambavyo tumeshuhudia
kufungiwa kwa video zisizopungua kumi kutokana na kudaiwa kuvunja
maadili.
Kwa
mujibu wa ripoti iliyoifikia nchi ambayo imeongoza kwa kufungia video
Afrika Mashariki ni Rwanda ikifuatiwa na Kenya kisha Tanzania.
Hii
video ya leo ni ya msanii wa Nigeria anaitwa Timaya akiwa na Mjamaica
Sean Paul kwenye remix ya bum bum ambayo imepokea maoni tofauti kwenye
mitandao mbalimbali baada ya hawa warembo kuonekana ndani yake
walivyovalia.
Video hii pia inaendelea kupata airtime kwenye vituo hata vya nyumbani Nigeria na sijaona taarifa zozote za kufungiwa.