Victoria Kimani yupo single.. atleast kwa muda huu – lakini kama mwanamke yeyote yule, naye anapenda siku moja aje kuwa mke wa mtu na mama wa watoto.
“Hauwezi tu kusema nimchague mtu na kusema ‘haya nimekuchagua wewe utakuwa mume wangu utakuwa baba wa watoto wangu’. Hivyo sivyo ninavyofanya. Nawish kama ingekuwa hivyo ningekuwa nishamchagua mtu…lakini siku hizi unatakiwa kuwa na connection na huyo mtu, anatakiwa kuwa anampenda Mungu anapenda familia yake. Na kwa wakati huu ni vigumu kumpata mtu wa aina hiyo,” aliongeza Victoria ambaye yupo jijini Dar es Salaam tangu wiki iliyopita.
Nataka mtu yeyote ninaem-date kuonesha anajivunia kuwa na mimi, anioneshe mapenzi, anipeleke sehemu zote, nataka awe ni mtu mwenye hisia kwa Mungu, awe mchapakazi na mbunifu kwenye mambo yake anayofanya. Mtu ambaye sio ana ratiba moja anayoifuata kila siku. Nataka mtu anaebadilisha ratiba huenda siku moja ananiambia twende tukapande mlima au twende tukaogelee baharini. Nataka kuwa na furaha na kupata starehe, nadhani watu wanapoanza kuzeeka ndipo wanapoanza kushangweka. Unapozidi kupata furaha ndivyo unavyozidi kubaki kijana milele. Kwa hiyo nataka yeyote ntakayekuwa nae nataka awe anapenda kushangweka, hata kama tukifikisha miaka 50 au 60.”
Victoria anasema ni rahisi kumjua mwanaume mwenye mapenzi ya dhati japo wasanii wapo pia.
“Unasoma ishara, kila wakati kuna ishara, nadhani utakuwa unafahamu kama mtu anakupenda kweli kwa sababu vitendo vinaongea zaidi ya maneno. Lakini wakati mwingine mtu anaweza kuonesha matendo lakini hawakupendi kwa hiyo inakuwa kama mchezo. Kwa hiyo inabidi kuomba, naamini katika maombi, naomba mara kwa mara ‘Mungu nioneshe kama kweli mtu huyu ananipenda au hapana’. Kwa kawaida ntafahamu ndani ya wiki mbili.”
Source: Times FM Website