Mwanamuziki wa kike ambaye ‘hips’ zake hazidanganyi anapocheza,
Shakira ameeleza kuwa chanzo cha kufanya video na Rihanna aliyemshika
kama mwanaume ‘Can’t Remember to Forget You’, ni wivu alionao boyfriend
wake Gerard Pique.
Katika mahojiano aliyofanya na jarida la Billboard, Shakira ameeleza
kuwa mchezaji huyo wa Barcelona hataki kabisa ashikwe na mwanaume kwenye
video na kwamba ni bora ashikwe na mwanamke mwenzake. Amesema kutokana
na kukataliwa na Gerard, hawezi kufanya video kama alivyozoea kufanya
awali na kwamba sasa inambidi afanye na wanawake.
“He’s very territorial, and since he no longer lets me do videos with
men, well, I have to do them with women. It’s more than implied in our
relationship that I can’t do videos like I used to.”
Video ya wimbo wa Shakira aliomshirikisha Rihanna ‘Can’t Remember to
Forget You’ ilikosolewa vikali katika nchi mbalimbali kwa madai kuwa
inahamasisha mapenzi ya jinsi moja.
Shakira na mcheza mpira huyo wamekuwa katika uhusiano tangu mwaka
2011, mwaka jana walijaliwa kupata mtoto wa kiume na wakampa jina la
Milan Pique Mebarak.
