DUNIA inalia, Tanzania inalia kutokana
na wimbi la biashara ya dawa za
kulevya, ambazo zinaleta madhara
makubwa kwa vijana ambao wengi wao
ndio hutumiwa kusafirisha na ndio pia
watumiaji wa dawa hizo zenye madhara
makubwa kiafya.
na wimbi la biashara ya dawa za
kulevya, ambazo zinaleta madhara
makubwa kwa vijana ambao wengi wao
ndio hutumiwa kusafirisha na ndio pia
watumiaji wa dawa hizo zenye madhara
makubwa kiafya.
Kwa mujibu wa takwimu, hivi sasa
duniani kuna watu milioni 15.9 kutoka
nchi 151, wanajidunga dawa za kulevya
aina mbalimbali kama vile kokeni,
heroine, amphetamines na nyingine
kama hizo, ambazo ni hatari kwa afya
zao.
Na kwamba watu milioni tatu kati ya
hao wanaojidunga dawa za kulevya
wamepata maambuziki ya virusi vya
Ukimwi na kwamba kasi ya maambukizi
ya virusi hivyo ni kubwa kwa watu
wanaojidunga sindano za dawa hizo
kuliko wale wanaotumia kwa njia ya
kuvuta au kunusa.
Shirika la Kimataifa la Medecins du
Monde (MdM), ambalo linashughulika na
kutoa misaada mbalimbali ya
kibinadamu ya hasa kwenye nchi na
maeneo yaliyoathiriwa na magonjwa,
vita, majanga ya asili, njaa na umasikini,
lipo pia Tanzania ambapo husaidia jamii
kwenye nyanja mbalimbali.

kazi za shirika hilo nchini
kwa shirika hilo MdM, kwa kuwa
tatizo la matumizi ya dawa za
kulevya nchini ni kubwa hivyo
wameanzisha mradi wa kupunguza
madhara kwa watumiaji wa dawa hizo.
Mradi huo uko kwenye nyanja tofauti
kama vile kutoa elimu kwa walengwa
kuhusu madhara na hatari ya matumizi
ya dawa hizo, kutoa ushauri na upimaji
wa virusi vya Ukimwi kuzuia na kutibu
maambukizi ya magonjwa ya ngono.
kulevya nchini ni kubwa hivyo
wameanzisha mradi wa kupunguza
madhara kwa watumiaji wa dawa hizo.
Mradi huo uko kwenye nyanja tofauti
kama vile kutoa elimu kwa walengwa
kuhusu madhara na hatari ya matumizi
ya dawa hizo, kutoa ushauri na upimaji
wa virusi vya Ukimwi kuzuia na kutibu
maambukizi ya magonjwa ya ngono.
Nyingine ni kuzuia, kuchunguza na
kutoa chanjo ya homa ya ini, kutoa
huduma za dawa za kupunguza makali
ya virusi vya Ukimwi kwa wale waliopata
maambukizi na ambao kinga zao
zimeshuka, kuzuia na kumudu uzidishaji
wa kiwango cha dawa za kulevya na
kupima na kutibu ugonjwa wa kifua
kikuu.
Kadhalika pia, MdM hutoa huduma ya
afya ya akili na msaada wa kijamii kwa
watu wenye matatizo ya akili
yanayotokana na matumizi ya dawa za
kulevya na pia kuwawezesha wale
walioamua kuacha kutumia dawa hizo
kuwa na elimu ya mafunzo ya
ujasiriamali ili kuwawezesha kiuchumi.
Matumizi ya dawa za kulevya nchini
katika hali ya matumizi ya dawa
za kulevya nchini,
bhangi ndiyo dawa ya kulevya ya
kwanza kuanza kutumika nchini. Pia
miaka ya 1980 dawa aina ya heroini na
kokeni za rangi ya kahawia zilianza
kutumika nchini na baadhi ya watu
kisha mwaka 1990, ndipo matumizi ya
dawa za kulevya kwa njia ya kujidunga
ikaanza.

Hata hivyo mapema mwaka 2000 dawa
za kulevya aina ya heroine nyeupe
ikaanza kuingia nchini na watumiaji
wakaendelea kuongezeka hata hivyo
anasema taarifa kuhusu watumiaji wa
dawa hizo ilipatikana kuwa watu
takribani 200,000 nchini wanatumia
dawa hizo.
Taarifa
ambazo sio rasmi kuhusu idadi ya
watumiaji wa dawa hizo hivi sasa
nchini, imeongezeka hadi kufika watu
kati ya 200,000 hadi 250,000 ndio
wanatumia dawa za kulevya. Aidha kati
ya watumiaji hao, watu 25,000
wanatumia dawa za kulevya kwa njia ya
kujidunga sindano za heroine na kati ya
hao 18,000 ni wakazi wa jiji la Dar es
Salaam, Tanzania.
Dawa za kulevya na aina
zake,
zimegawanyika katika makundi matatu.
Kundi la kwanza ni dawa za kulevya aina
ya kichangamshi. Ambavyo ni pamoja na
kafeine, cola majani ya chai, kahawa,
kokeni, nicotine (sigara). Na kwamba
katika kundi hili zipo dawa ambazo ni
halali kwa matumizi kama vile chai,
kahawa, cola na hata sigara.
watumiaji wa vichangamshi
hivyo mwili huchangamka, kupata
nguvu, kusikia hamu ya kufanya jambo
na kwamba kwa watumiaji wa dawa
hizo kwa muda mrefu, wakikosa
hushindwa kufanya jambo hadi hapo
watakapozipata. Madhara ya
vichangamshi hivyo ni pamoja na
mapigo ya moyo kuongezeka, damu
kuzunguka kwa kasi, mboni za macho
kuwa kubwa na mtumiaji huhisi njaa
kila wakati na hukosa usingizi.
“Unajua wapo watu wanaosema bila
kunywa kahawa siwezi kufanya kazi, ni
kweli ndani ya kahawa kuna dawa za
kulevya ambazo humfanya mtu
achangamke, unapotumia kwa muda
mrefu unakuwa addict”,
Kundi la pili ni dawa za kulevya
ziitwazo vipumbaza.
Mtumiaji wa dawa hizo hupunguza
uwezo wa kufikiri, uwezo wa kufanya
maamuzi nao hupungua na dawa
kwenye kundi hili ni pamoja na vilevi,
heroine, morphine, methadone,
benzodiazepines na barbiturates. Na
kwamba kati ya dawa hizo zipo halali
ambazo hutumika viwandani kama vile
methadone na kwamba nyingine ni
haramu.
Madhara kwa watumiaji wa dawa
kwenye kundi hili ni pamoja na mapigo
ya moyo kushuka, damu kuzunguka
taratibu mwilini, kupoteza fahamu,
mboni za macho kusinyaa. Kundi la tatu
ni vileta njozi, ambazo ni dawa kama vile
bhangi na aina fulani ya uyoga.
Watumiaji wa dawa hizi hupata hisia za
kufanya jambo au kuhisi yuko mahali au
eneo fulani.

Madhara ya dawa hizo ni kwamba
hufungua ubongo na kumfanya
mtumiaji kuwa na hisia tofauti kama vile
kuhisi yuko nchi nyingine, kuona
dimbwi la maji kama ni bahari, kumuona
mtu mwembamba kuwa ni mnene. Pia
watumiaji wa dawa hizi huwa na hisia
ya kufanya mambo bila ridhaa yao kama
vile kufanya ngono.
Madhara kwa ujumla Kwa mujibu wa
MdM madhara ya matumizi ya dawa za
kulevya ni makubwa, kwani idadi ya
watumiaji wa dawa za kulevya
inaongezeka na hiyo inatokana na
kwamba kazi ya kudhibiti dawa hizo ni
ngumu sio tu kwa Tanzania bali duniani.
Hivyo, njia mbadala zinatumika
kupunguza madhara kwa watumiaji,
ikiwa ni pamoja na kuwa na miradi
kama hiyo ya kupunguza madhara kwa
watumiaji wa dawa za kulevya.
sababu za kwa nini watumiaji wa
dawa wa kulevya wengi hawaachi,
Tafiti zinaonesha
kwamba kwenye vitu vinavyompa mtu
raha sio rahisi kumwambia aviache.
“Ni ngumu sasa kumwambia mtu aache
kutumia dawa za kulevya, kwani ni kitu
kinachogusa hisia na kinampa raha, ila
mbinu mbadala ni kumsaidia kupunguza
madhara na kama akiona haina faida
ataamua mwenyewe kuacha, ila sio kwa
kumwambia ni kwa kumuelimisha tu”,
Tanzania watumiaji
wengi wa dawa za kulevya hutumia
heroine kwa kuwa ni rahisi na hata
upatikanaji wake na hutumika kwa njia
ya kujidunga sindano. Kwa hapa nchini
watumiaji wa dawa hizo ni wanaume
kwa wanawake, na kwamba kundi
kubwa la vijana ambao ndio nguvu kazi
ya taifa, wengi wao ndio walioathirika
zaidi na dawa hizo.

Kete moja ya heroine huuzwa shilingi
1,000 ukilinganisha na kete moja ya
kokeni ambayo huuzwa kati ya shilingi
7,000 hadi 10,000 hivyo watumiaji wake
ni watu wenye uwezo. Madhara ya dawa
hizo ni nguvukazi kupotea, vifo,
ongezeko la maambukizi ya virusi vya
ukimwi, homa ya ini na pia nchi kutumia
fedha nyingi kupiga vita biashara hiyo
haramu inayoua taratibu ralisimali watu.
Jinsi mtu anavyoweza kuacha
kutumia dawa za kulevya, moja ya waelimisha
rika, toka shirika la MdM, anasema
alitumia dawa hizo kwa miaka tisa, na
kwamba mradi huo wa kupunguza
madhara ulipoanzishwa alishiriki na
yeye mwenyewe kuamua kuacha.
“Nilikuwa nafika hapa MdM
wanatutunza na kutuelimisha kwa
kutupa vifaa salama kama mabomba ya
sindano ambayo ni mapya hivyo kule
kushirikiana mabomba nikaacha, halafu
kidogo kidogo nikaanza kuona hakuna
faida ya kuendelea kujidunga heroine,
nikaamua mwenyewe kuacha , hivi sasa
ni miaka mitatu imepita tangu niache”,
anasema Divai moja wa walioacha kutumia madawa hayo.
Dawa za kulevya ni hatari ila
tatizo ni jinsi ambavyo linateka hisia na
akili za watumiaji na kwamba sio jambo
la kumwambia mtu aache, bali ni uamuzi
wa mtu binafsi kutoka moyoni kwani si
rahisi kuelewa raha au hisia za mtu
anayetumia dawa hizo, ingawa kuna
madhara makubwa lakini, jambo
muhimu ni kuwasaidia watumiaji
kupunguza madhara, na wakiona yafaa
wataacha wenyewe.

Nini Kifanyike cha kufanya
katika mapambano dhidi ya dawa hizo
haramu,
kutokomeza
kabisa matumizi ya dawa hizo ni ngumu
kama ilivyo kwenye nchi nyingine
duniani, kwani ni kitu kinachogusa hisia
na kumletea mtumiaji raha ambayo si
rahisi kwa asiyetumia kuifahamu, lakini
cha kufanya ni kuwasaidia watumiaji
kuwakinga na madhara ya dawa hizo.
kabisa matumizi ya dawa hizo ni ngumu
kama ilivyo kwenye nchi nyingine
duniani, kwani ni kitu kinachogusa hisia
na kumletea mtumiaji raha ambayo si
rahisi kwa asiyetumia kuifahamu, lakini
cha kufanya ni kuwasaidia watumiaji
kuwakinga na madhara ya dawa hizo.
kikubwa ni kuwafikia na
kuwaelimisha kuhusu madhara na
kuwapa ushauri nasaha na kuwasaidia
kutoshirikiana bomba la sindano na
wenzao ili kuepuka maambukizi ya
magonja kama virusi vya ukimwi na
homa ya ini na pia kuwasaidia kuwapa
tiba mbadala ya Afya, tiba ya afya ya
akili na kuwasaidia wasizidishe kiwango
cha dawa hizo.

Na kwamba ikiwa watapata msaada
kama huo, na iko siko wao wenyewe
kwa wataona umuhimu wa kuacha,
kwani suala la kuacha ni uamuzi wa
ndani wa mtu na si kuwalazimisha ,
kutokana na jambo hilo kuwa gumu
kwa hali ya kawaida kuliko jinsi
ambavyo watu wanadhani.
kama huo, na iko siko wao wenyewe
kwa wataona umuhimu wa kuacha,
kwani suala la kuacha ni uamuzi wa
ndani wa mtu na si kuwalazimisha ,
kutokana na jambo hilo kuwa gumu
kwa hali ya kawaida kuliko jinsi
ambavyo watu wanadhani.