Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van Der Pluijm.
Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van Der Pluijm amesema pamoja na kusafiri
leo Jumamosi, lakini lazima waupime uwanja watakaochezea mechi leo.
Pluijm raia wa Uholanzi amesema ni jambo la msingi kwao kufanya mazoezi kwenye uwanja huo, hivyo lazima.
Yanga imeanza safari leo hii asubuhi kwenda Alexandria, mwendo wa saa mbili kutoka hapa Cairo.
“Baada ya kufika Alexandria, lazima usiku tutafanya mazoezi kwenye uwanja tutakaochezea mechi.
“Kufanya hivyo kunakusaidia kuujua uwanja, ikiwa ni pamoja na vipimo vyake.
Ni jambo la msingi sana hata kama hayatakuwa mazoezi ya muda
mrefu,” alisema.Yanga, kesho itashuka kwenye uwanja huo kuwavaa mabingwa
wa Afrika Al Ahly ambao katika mechi ya kwanza waliwafunga bao 1-0.