Siku ya Wapendanao siyo kwa ajili ya kufanya ngono au uzinzi.Hii ni siku
inayolenga kuimarisha upendo kati yako na mtu mwingine yeyote.
Nchini Italia wakati huo kulikuwa na kiongozi
aliyeitwa Mfalme Claudius II; aliamini kuwa askari anapooa hawi
mkakamavu na pia muda mwingi anawaza kuhusu familia yake zaidi ya kitu
kingine chochote. Hivyo alipiga marufuku ndoa kwa askari.
Kitendo hicho hakikuwafurahisha watu wengi,
akiwamo Padri Valentino. Kiongozi huyu wa kidini aliendelea kufungisha
ndoa kwa siri. Mfalme Claudius alipopata habari hizi aliamuru Valentino
akamatwe na kuuawa. Mtakatifu Valentino aliuawa siku na tarehe kama ya
leo, ndiyo maana ikatangazwa rasmi kuadhimishwa kwa ajili ya kumkumbuka
kama Baba wa Upendo na mtetezi wa wanandoa. Historia zinaonyesha kuwa
aliyetangaza rasmi kuadhimisha siku hiyo ni Papa Gelasius.
Aidha, iko simulizi nyingine inayosema kuwa akiwa gerezani Valentino aliandika barua ambayo ilikuwa na salamu za Valentino kwa binti aliyekuja kumsalimia gerezani; mwisho wa barua alihitimisha kwa kusema ‘Kutoka kwa Valentino wako’.
Tangu hapo Valentino anakumbukwa kama mtetezi wa wapendanao na sikukuu yake kuadhimishwa ulimwenguni kote.
Aidha, iko simulizi nyingine inayosema kuwa akiwa gerezani Valentino aliandika barua ambayo ilikuwa na salamu za Valentino kwa binti aliyekuja kumsalimia gerezani; mwisho wa barua alihitimisha kwa kusema ‘Kutoka kwa Valentino wako’.
Tangu hapo Valentino anakumbukwa kama mtetezi wa wapendanao na sikukuu yake kuadhimishwa ulimwenguni kote.
ZAIDI KUHUSU SIKU HII
Siku hii inaonekana ni maalumu kwa ajili ya
kuonyeshana upendo wa dhati kwa mtu yeyote. Ni siku muhimu na yenye
maana kubwa kwa kila mtu, maana upendo hauchagui.
Ingawa wengine wanaweza kuitumia au kuichukulia
kwa kadri wanavyotaka, msingi wa siku hii hasa ni kuonyesha upendo kwa
watu, si lazima awe mke au mumeo ama mchumba.
Maana na ukweli wa uwepo wa siku hii inayoitwa
Valentine’s Day inaharibiwa na baadhi ya watu kwa kuiona kama ni siku ya
kufanya ngono/uzinzi. Ukitaka kuthibitisha hili, siyo lazima uende chuo
kikuu ili kupata ujuzi wa kujua ukweli, bali tembelea nyumba za wageni
zilizo karibu, nyingi utakutana na bango ‘vyumba vimejaa!’
NAMNA INAVYOPASWA
Msingi hasa wa siku hii ni kuonyesha upendo, hii
ina maana kuwa unaweza kuonyesha upendo kwa yeyote iwe ni jirani, mzazi
au yeyote unayempenda, siyo lazima mpenzi kama ambavyo baadhi ya watu
wanafanya.
Waweza kumtumia ujumbe mzuri mtu yeyote
unayempenda au hata zawadi, waweza kutembelea yatima, wagonjwa na hata
watu wengine wowote; kubwa hasa kwa siku hii ni kuonyesha upendo.
Hata hivyo, kwa sababu ya ukweli kwamba wengi
wanaiona kama ni siku ya ngono, ni suala la msingi sana unapotoa zawadi
kwa mtu wa jinsi tofauti kuwa makini; angalia zawadi unayoitoa isije
ikaharibu siku yako na maisha yako kwa jumla badala ya kukupa furaha,
kwa sababu baadhi ya wenza wa wale ambao unaweza kuwapa zawadi wanaweza
kutafsiri kama wewe una uhusiano wa kimapenzi na mtu huyo.
Wataalamu mbalimbali wa masuala ya uhusiano,
wanasema katika siku kama hii ya leo, ni vizuri walio kwenye uhusiano
mbaya kujifunza namna ya kuwa na uhusiano mzuri, kwani ubaya hauna maana
katika maisha.
“Hii ni siku muhimu kwa kila mtu kuangalia
uhusiano wake na watu wanaomzunguka,” anasema Hi Song, ambaye ni
Mtaalamu wa Masuala ya Uhusiano nchini Marekani kutoka Kituo cha Ushauri
cha Marriage Life. Anasema kuna ambao huanzisha uhusiano siku hiyo kwa
lengo la kupata mtu wa kustarehe naye, hili ni kosa. Kama mtazamo wako
ni kutafuta mpenzi mpya na kwenda kustarehe naye utakuwa unakosea sana.
Haina maana ya ngono wala anasa na kuharibu fedha kwenye ulevi. Yapo
mengi ambayo unaweza kuyafanya kwa lengo la kuifanya siku yako kuwa
nzuri.
-Chanzo; mwananchi.
-Chanzo; mwananchi.