Video Queen Agnes Jerald ‘Masogange’akikata mauno.
Weekly Star Exclusive ilimbamba mrembo huyo juzikati nyumbani kwa
mwigizaji Salma Jabu ‘Nisha’, Kijitonyama jijini Dar ambapo Nisha
alikuwa akipiga makofi na kushangilia wakati Masogange alipokuwa akikata
mauno.
Agnes Jerald ‘Masogange’ akiwa nyumbani kwa Salma Jabu ‘Nisha’, Kijitonyama jijini Dar
“Sijacheza siku nyingi jamani ndiyo maana leo nimejikumbushia mambo
yangu ya mjini, kuna vitu vingi sana nilivimisi kama kukutana na watu
hivi na kucheka pamoja kwa uhuru,” alisema Masogange.Wakati akiendelea kukatika, mtoto mdogo ambaye jina lake halikupatikana mara moja mwenye umri uliokadiriwa kama miaka 7, alishangilia na kucheza naye pamoja.
Tangu arejee kutoka Bondeni, Masogange amekuwa shosti mkubwa wa Nisha ambapo mbali na urafiki, wanafanya filamu pamoja iitwayo Betina na Zena.
Kwenye msala wa madawa ya kulevya, Masogange aliachiwa kwa kulipa faini baada ya kuthibitika kuwa mzigo aliokutwa nao haukuwa madawa ya kulevya bali ni ‘material’ ya kutengenezea madawa tofauti.