WASHIRIKI EBSS WAMPA 5 MADAM RITA

 
Melisa John akiwa katika pozi ndani ya hoteli (jina kapuni) pande za Mbezi Beach jijini Dar. Mpigie kura kwa kuandika neno (kura) acha nafasi andika namba 22 kisha tuma kwenda namba 15530.

 
Elizabeth Mwakijambile akiwa katika pozi, mpigie kura kwa kuandika neno (kura) acha nafasi andika namba 8 kisha tuma kwenda namba 15530.
 
Maina Thadei (21)
“Napenda sana EBSS, nampenda Madam Rita siyo kwamba najipendekeza, nasema ukweli wa moyo wangu sitasahau siku ambayo nilichaguliwa kujiunga na EBSS bila madam Rita mimi si chochote,” alisema Maina.
 
Amina Chibaba akijiachia kambini hapo, mpigie kura Amina kwa kuandika neno (kura) kisha acha nafasi andika namba 03 kisha tuma kwenda namba 155.
 
Mandela Nicholas mkubwa kuliko wote kiumri akiwa katika pozi kama la Mwanamziki wa Marekani hayati Michael Jackson,  mpigie kura Mandela kwa kuandika neno (kura) kisha acha nafasi andika namba 10 kisha tuma kwenda namba 15530
 
Emmanuel Msuya akipiga gitaa mbele ya mwandishi wa habari, , mpigie kura Emmanuel kwa kuandika neno (kura) kisha acha nafasi andika namba 21 kisha tuma kwenda namba 15530
 
Washiriki wa Bongo Star Search wakiwa katika picha ya pamoja kambini Mbezi Beach jijini Dar.
Habari, Picha na Jelard Lucas/GPL
WASHIRIKI wa Epiq Bongo Star Search ‘EBSS’ chini ya uzamini wa gazeti la Championi wamempongeza Mkurugenzi wa mtendaji wa kampuni ya Bench mark production Rita Poulsen ‘madam Rita’ kwa kutambua vipaji vya mziki kwa vijana wa kitanzania
Wakiongea na mwandishi wa gazeti la Championi jioni ya leo wamesema madam Rita ni mwanamke jasili Tanzania kwani amejitolea kutambua vipaji vyao na wengine wanashukuru Mungu kufikia pale walipo kwani wengi hawakutarajia kuingia top 6
Wasikilize washiriki hawa wakiwa kambini Mbezi Beach jijini Dar.
Wasikilize washiriki hawa wakiwa kambini Mbezi Beach jijini Dar.
Melisa John (22)
“Nampongeza sana Madam kwa kujua na kuvumbua vipaji vyetu, ni mwanamke jasili asiyerudi nyuma kupambana na vipaji vyetu, hapa kambini ni zaidi ya elimu, mafunzo na maisha mengine bila yeye tusingekuwa hapa, tunafanya mazoezi mengi,” alisema Melisa
Elizabeth Mwakijambile (21)
“Jamii lazima iheshimu mchango wa mwanamke huyu, kiukweli ni zaidi ya mama, anatufanya tujifunze mambo mengi, nimejifunza mengi, bila yeye ningepata hii elimu niliyoipata hapa, big up madam Rita,” alisema Elizabeth
Maina Thadei (21)
“Napenda sana EBSS, nampenda Madam Rita siyo kwamba najipendekeza, nasema ukweli wa moyo wangu sitasahau siku ambayo nilichaguliwa kujiunga na EBSS bila madam Rita mimi si chochote,” alisema Maina
Amina Chibaba (22)
“Sikuwahi kuota kama naweza kuonekana kwenye shindano kama hili, wakati naanza, madam Ritha amekuwa nguzo imara kwangu, sina cha kumpatia isipokuwa Mungu ampe uhai siku zote, napenda vitu vyote hapa kambini kwasababu madam amefanya kazi kubwa kutuandalia mahala pazuri kwa kujifunzia,” alisema Amina
Mandela Nicholas (25)
“Madam Rita ni mwanamke shupavu, ametusaidia sana kutupatia ushauri hasa kutokata tama na kujiamini kwamba tunaweza siku zote, namshukuru sana Madam Rita na huyu ni mfano kwa wanawake wengine Tanzania,” alisema Mandela
Emmanuel Msuya (23)
“Nakumbuka kauli yake madam Rita ya kwamba usikubali kutawaliwa na neon ‘HAPANA’ sema unaweza na usonge mbele, yeye amekuwa mtu pekee anayenitia moyo kujumuika na wenzangu katika utendaji kazi za EBSS, nampongea kwa mchango wake,” alisema Msuya
Wapigie kula washiriki hawa ili kuwawezesha kuibuka kidedea kwenye fainali zitakazofanyika Novemba 30 mwaka huu, ili kushiriki katika ukumbi wa Escape One Mikocheni jijini Dar.
back to top