AUNTY LAIVU NA MUMEWE CHUMBANI

MCHEZA sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel amejianika laivu mtandaoni kwa mara ya kwanza akiwa chumbani amelala na mumewe, Sunday Demonte, Dubai anakoishi mwanaume huyo huku msanii huyo akiwa na maskani yake jijini Dar.

Aunt Ezekiel akiwa na mumewe, Sunday Demonte chumbani.
Aunt alitundika picha tatu kwenye ukurasa wake katika Mtandao wa Instagram akiwa na Demonte huku akisindikizia na maneno ya kumsifia laaziz wake huyo kwa kuwa ilikuwa siku ya kuzaliwa kwake (Demonte).
Baada ya tukio hilo, mashabiki wake walimmwagia sifa kemkemu kuwa watu wamekuwa wakimsema vibaya kwa kukaa mbali na mumewe lakini sasa amewaziba midomo.
back to top