Wachezaji
wa Arsenal Aaron Ramsey (kulia) na Mesut Ozil wakishangilia bao lao la
pekee dhidi ya Dortmund. Bao hilo limefungwa na Ramsey dakika ya 62.
Mshambuliaji wa Chelsea Samuel Eto'o akishangilia na kocha wake Jose Mourinho baada ya kuifungia timu yake bao.
Lionel Messi (kushoto) akishangilia moja ya mabao aliyoifungia timu yake ya Barcelona na Cesc Fabregas.
Arsenal, Chelsea na Barcelona zimeibuka na
ushindi katika mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya zilizopigwa usiku huu.
Arsenal wameilaza Borussia Dortmund bao 1-0, Chelsea wakiizamisha 3-0
timu ya Schalke 04 wakati Barcelona wakiichachafya AC Milan bao 3-1. Bao
la Arsenal limefungwa na Aaron Ramsey ya Chelsea yakiwekwa kimiani na
Samuel Eto'o aliyefunga mawili na Demba Ba wakati ya Barcelona
yakifungwa na Lionel Messi aliyefunga mawili na Sergio Busquets na lile
la AC Milan Gerard Pique aliyejifunga.