Irene Pancras Uwoya.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Utafiti na Masoko wa Clouds Media Group,
Ruge Mutahaba, katika harakati za vipindi hivyo, alianza Wema kwa
kuanzisha ‘aidia’ ya kipindi kipya kiitwacho In My Shoes ambacho
kitaanza kuoneshwa kuanzia Alhamisi hii, saa tatu na nusu usiku kupitia
Clouds TV.
Wema Isaac Sepetu.
Alisema baada ya Wema kutengeneza kipindi hicho na kupata maoni
mengi, Uwoya akajibu mapigo kwa kuanzisha cha kwake kinachoitwa Paradise
ambacho kitakwenda hewani Jumanne hii (kesho).“Mashabiki wa Clouds TV watapata kuona vita ya kibiashara, Uwoya atakuwa akionekana katika kipindi hicho ambacho kitakuwa kinahusu upakaji rangi katika nyumba za watu mbalimbali huku Wema naye akikimbiza katika In My Shoes,” alisema Ruge.
chanzo; http://www.globalpublishers.info/