SELLY AMUOMBA MSAMAHA MPENZI WAKE KWA KUFANYA MAPENZI NA NANDO NDANI YA BIG BROTHER
Hatimaye mshiriki wa Ghana katika reality show ya Big Brother ‘The
Chase’ Selorm Galley maarufu kama Selly aliyetoka wiki moja iliyopita,
amemuomba msamaha boy friend wake (wa Ghana) kwa yale aliyoyafanya
mbele ya Camera za nyumba ya Big Brother.Kupitia kipindi cha live ‘Celebrity Show’ cha ETV ya Ghana Selly
ambaye pia ni muigizaji alianza kwa kumshukuru mpenzi wake Praye Tietia,
na kutokana na kwamba kuna uwezekano yaliyomkwaza mpenzi wake ni mengi,
Selly alimuomba msamaha kwa yale yote yaliyojiri mjengoni (ikiwemo
kufanya mapenzi na Nando) alipokuwa anaiwakilisha nchi yake kuzifukuzia
$300,000.
Selly mwenye miak 25 alisema “I am very thankful for the
opportunity given me. I want to thank my boyfriend, Praye Tietia and
also use this opportunity to say I am very sorry (for all that
happened)”, na akasisitiza “I am very sorry”.
Selly amekuwa akiandamwa na maneno mengi toka camera za Big Brother
zimnase akifanya mapenzi na aliyekuwa mwandani wake katika The chase
Nando, kitendo kilichowaudhi zaidi mashabiki wa nchini kwake Ghana ambao
wamekuwa wakimuandama kupitia mitandao ya kijamii.