BAADHI ya mastaa wa filamu na muziki kwa kushirikiana na uongozi wa Clouds Media Group, wamejitolea kujengea kaburi la gwiji wa muziki wa taarab, marehemu Fatma Binti Baraka ‘Bi. Kidude’.
Tukio hilo lilifanyika hivi karibuni katika makaburi ya Kitumba Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar ambapo timu ya wasanii Kulwa Kikumba ‘Dude’, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Raheem Nanji ‘Bob Junior’ walijitolea vifaa vya ujenzi yakiwemo matofali ya kujengea.
Bi. Kidude aliyekuwa mahiri wa kuimba nyimbo za taarab, alipatwa na mauti Aprili 7, mwaka huu baada ya kusumbuliwa na maradhi ya sukari, mapafu na figo kwa muda mrefu.