Ulimis? video na maelezo ya Linah akizungumza kuhusu kubakwa.

linah2 
Kama hii stori ilikupita au uliisikia kijuujuu hii post inakuhusu….. baada ya stori kuenea kwamba mwimbaji Linah amebakwa baada ya kuzidiwa na kilevi usiku akitoka club, mwenyewe amezungumza na millardayo.com
Kama utashindwa kutazama hiyo video hapo chini, haya ni yale muhimu aliyoyasema…… ‘mi
mwenyewe nimezisikia hizo habari na zimenishtua lakini katika kuja kufatilia nikagundua kwamba majina yamegongana, kuna mtu mwingine anaitwa Linah ambae amepatwa na hilo jambo, sikutoka nyumbani kwa siku tatu… yani nilikwenda tu movie na kurudi nyumbani, katika kufatilia nilimnukuu mtu alieniambia kwamba rapper Kalapina alikua ameziandika facebook ila sio Linah mimi, usumbufu nimepata mkubwa sana mpaka nyumbani wamenipigia simu, wengine walivyosikia tu ndio wameanza kunilaumu bila kufanya uchunguzi na kunionya kwamba Wasanii acheni ulevi, watu wasianze tu kwa kulaumu’
back to top