FEZA AONGOZA KUCHUKIWA NA WENZAKE NDANI YA JUMBA LA BIG BROTHER...!
Habari mbaya kwa Tanzania, Feza Kessy ni miongoni mwa washiriki watatu
waliopigiwa kura zaidi kutoka wiki hii...FEZA amepata kura nyingi zaidi
hii inaonyesha kuwa ndio mshiriki anayechukiwa zaidi ndani ya jumba
hilo...
Feza ameungana na mpenzi wake Oneal na Elikem kwenye kikaango
hicho cha eviction. Wa kwanza kumtaja Feza kwa kudai kuwa ni mbeya na
jinsi anavyopenda kuwakusanya washiriki wenzake na kuwashawishi mi
Msouth, Angelo.
Beverly wa Nigeria pia amemtaja Feza kwa madai kuwa ana upinzani mkali kwenye shindano hilo.
Elikem
amewataja Oneal na Feza huku Cleo wa Zambia akimtaja Feza kwa madai
kuwa ni tishio kubwa kwake na kusema wazi kuwa hataki kumuona Feza
anaondoka na dola laki tatu.
Haya sasa muda wa kuanza kumpigia kura Feza Kessy asitoke ndio huu