BBA: MSHIRIKI WA TANZANIA ( NANDO) HUENDA AKASHITAKIWA KWA KOSA LA KUMDHALILISHA MSHIRIKI WA KIKE TOKA GHANA
Mshiriki wa pekee katika Jumba la BBA
The Chase , Selly kutoka nchini Ghana, amesema ya kwamba yupo mbioni
kumfungulia mashtaka mshiriki kutoka nchini Tanzania Nando kwa kitendo
cha kumdhalilisha na kumsingizia amemuambukiza Ugonjwa wa Zinaa.Baada
ya kutolewa katika jumba hilo wiki iliyopita, Selly ameshauriwa na mama
yake na tayari wamewasiliana na Waandaji wa Shindano hilo. " Nimepima
sijakutwa na maambukizi ya aina yoyote ya Magonjwa ya Zinaa wala sina
historia hiyo" Alisema Selly.
" Mimi na Nando hatukufanya Mapenzi
zaidi ya kucheza tu Kitandani, nashangaa hata kwa kiasi gani mambo
yamekuwa hivi" Aliongeza Mrembo huyo.