MSHIRIKI WA TANZANIA ( FEZA KESSY) KATIKA BIG BROTHER YUKO HATARINI KUTOLEWA...KURA ZAKO ZINAHITAJIKA

Kama hisia za wengi zilivyokuwa kuhusiana na Betty kulipiza kisasi, mambo yameenda hivyo.. Betty ambaye ni Head of House wa Diamond house amemuokoa Bolt na kumuweka kikaangoni Feza..

Katika Ruby house, Selly ambaye ni Head of house huko, naye ametumia ukuu wake wa kaya kumuokoa Biguesas na kumtia kitanzini Koketso..

Wiki hii Feza, Dillish, Hakeem, LK4 na Koketso wako kikaangoni..

Wakati wa kupiga kura kwa nguvu zote umewadia.. Kazi kwetu watanzania kumpigia kura wakwetu..

Tuwahimize pia marafiki zetu Africa kumpigia kura Feza kwani kura zao ni muhimu sana.. -- Kila nchi inahesabiwa kama kura moja.

Kupiga kura tembelea -->bigbrotherafrica.dstv.com
back to top