Habari zisizokuwa na chenga kutoka kwa chanzo chetu ambacho ni mtu wa
karibu wa mrembo huyo, zilieleza kwamba kufuatia hali hiyo, Penny
alikimbizwa kwenye Hospitali ya Regency, Dar wikiendi iliyopita kisha
akalazwa, akachomwa sindano na kutundikiwa dripu.
Hata hivyo, habari
tulizozipata wakati tunakwenda mitamboni zilieleza kuwa Penny
aliruhusiwa kutoka hospitalini na anaendelea vizuri.
Akizungumzia hali hiyo, Penny aliliambia gazeti hili kuwa ni kweli
alizidiwa usiku na alikimbizwa hospitali ambapo pamoja na mengine lakini
kubwa vipimo vilionesha kuwa alikuwa na malaria.