MAN CITY WAANZA BALAA LA USAJILI - MBRAZIL FERNANDINHO YUPO MANCHESTER KWA VIPIMO
Fernandinho amewasili jijini Manchester
kwa ajili ya kukamilisha vipimo vya afya ili aweze kukamilisha usajili
wake wa kujiunga na klabu ya Manchester City akitokea Shakhtar Donetsk.Kiungo huyo mwenye miaka 28 anaweza kuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa chini ya utawala mpya wa kocha Manuel Pellegrini.
Mbrazil huyo aliisadia Shakhtar kubeba
ubingwa wa Ukraine msimu uliopita na sasa anahamia Manchester City ili
kuweka hai ndoto yake ya kuiwakilisha Brazil kwenye michuano ya Kombe la
Dunia mwaka ujao.
Mapema leo mchana Mbrazil huyo alionekana akiingia kwenye hosptali a Bridgewater tayari kukamilisha usajili wake.