HUDDAH TOKA KENYA AYAAGA MASHINDANO YA BIG BROTHER..... MWAKILISHI WA TANZANIA ALIA NA WAVUTA BANGI
Maneno huumba....!!! Huddah ameliaga shindano hilo...
------------------------
Huddah
ambaye ni mshiriki kutoka Kenya alijikuta akibubujikwa na machozi jana wakati
akimuelezea Angelo (SA) kuhusiana na uhusiano wake wa kimapenzi ambao
ni wa ku-beep yani vuta nikuvute ambao amekuwa nao nchini kwao.
Mrembo huyo hakutaja jina la mpenzi wake lakini inahisiwa
alimaanisha kuwa katika mahusiano na Rapper Prezzo wa Kenya. Kwa muda
sasa kumekuwa na umbea mtaani kuhusiana na uhusiano wa kimapenzi kati ya
wawili hao lakini haijafahamika kinaga ubaga kama Huddah alimaanisha
kum-miss Mr. President. ..
Mrembo huyo akizidi kufunguka, alielezea jinsia
anavyo-miss mabusu motomoto, anavyo-miss kung'atwa shingoni n.k. “I miss
the way that he kisses me. I miss him biting my neck”..
LEO MACHOZI YAKE YAMELIPWA BAADA YA MREMBO HUYO KUONDOLEWA NDANI YA JUMBA HILO....Mashabiki wamepiga kura ya kumwondoa ili asiendelee kumlilia mpenzi wake.....
Mshiriki mwingine aliyeaga mashindano hayo ni Denzel wa Uganda....
KWA UPANDE MWINGINE, mrembo wa Tanzania ,Feza anayeiwakilisha Tanzania alijikuta
katika simanzi kali wakati alipoelezea kuhusu jinsi ambavyo kaka yake
aliteseka kutokana na kujihusisha na madawa ya kulevya .. 'drugs'.
Feza alitumia fursa hiyo
kuwasihi watu hasa vijana kujiepusha kabisa na madawa ya kulevya kwani
ni hatari sana katika jamii inayotuzunguka..