BABA YAKE DIAMOND YUPO HOI ANAUMWA......DIAMOND HAJAWAHI KANYAGA KUMJULIA HALI
BABA wa msanii Nasibu Abdul ‘Diamond’, Abdul Juma yupo hoi akisumbuliwa na ugonjwa wa miguu.
Kwa
mujibu wa chanzo makini, Baba Diamond anasumbuliwa na tatizo la miguu
kuvimba hali ambayo imemfanya ashindwe kutembea lakini cha kushangaza
mwanaye, Diamond hajaenda kumjulia hali.
“Baba Diamond ni mgonjwa kwa muda mrefu sana lakini Diamond hajawahi kuja kumuona hata siku moja,” kilisema chanzo hicho.
Baada
ya kuzinyaka habari hizo, waandishi wetu walifunga safari mpaka
nyumbani kwa mzee huyo, Magomeni-Kagera, jijini Dar ambapo alikiri
kuugua kwa muda mrefu na kukosa msaada kutoka kwa Diamond. “Nasumbuliwa
na miguu kwa muda mrefu sana na ninatibiwa katika Hospitali ya Saint
Monica, Manzese-Darajani. Diamond ana taarifa za kuumwa kwangu lakini
hajawahi kuja kuniona.
“Namshukuru mwanangu Queen Doreen kwa kunijali kwa kila kitu,” alisema baba Diamond.