|
Samba SC
v/s
Jeshi la
Oman
|
Mabingwa wa soka Tanzania, Simba SC walifungwa mabao 3-1 katika mechi ya kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Jeshi la Oman.
Mechi hiyo
ilichezwa Ijumaa jioni kwenye uwanja wa Qaboos complex jijini Muscat.
Bao la simba
lilifungwa katika kipindi cha pili na Haruna Moshi 'boban'.
|
Mwenyekiti
wa Simba Ismail Aden Rage
akiwa na wenyeji wake huko Oman
wakiangalia
Simba ikisurubiwa
na wanajeshi.
|
Mwenyekiti
wake Ismail Aden Rage alikuwa jukwaani pamoja na viongozi wengine wa Simba,
Rahma Al Kharusi na Musleh Rawahi pamoja na kocha Talib Hilal wakiishuhudia
simba ikizama mbele ya wanajeshi hao ambao kikosi chao kina wachezaji tisa
wanaocheza timu ya taifa ya Oman.
|
Boban na
wenzake wakishangilia goli
lao 1-3 katika mchezo huo.
|
|
Wachezaji Kaseja,
Mwinyi Kazimoto, Mrisho Ngassa, Sunzu wakiwa benchi huku wakizungumza na
mfadhili wa safari yao Bi.Rahma na mwenyekiti wao Aden Rage.
|
|
Simba SC 1 - 3 Timu la Jeshi la Oman.
|